Wednesday 13 April 2016

GETAFE YAMTIMUA KOCHA WAKE ESCRIBA


Timu ya Getafe imetangaza kumuondoa kocha wake Fran Escriba kutokana na matokeo yasiyoridhisha kwenye ligi kuu ya soka ya La Liga nchini Uhispania.

Katika mechi 12 za mwisho, Getafe imeweza kukusanya pointi 2 pekee kwa kutoa sare mechi mbili huku ikicharazwa mechi kumi.

Mara ya mwisho Getafe ilishindwa na Villareal 2-0 mwishoni mwa juma lililopita na kuning'inia katika nafasi ya 19 kwa pointi 28.


Nafasi ya Escriba huenda ikachukuliwa na kocha Joaquin Caparros ambaye aliwahi kufunza Sevilla, Athletic Bilbao, Mallorca na Granada.

No comments: