Wednesday 20 April 2016

OLYMPIQUE MARSEILLE YAMTIMUA KOCHA WAKE MICHEL.

Olympique Marseille yamtimua kocha wake Michel

Kilabu ya Olympique Marseille inayocheza kwenye ligi kuu ya soka ya Ligue 1 nchini Ufaransa imemtimua kocha wake Michel.

Kilabu hiyo ilitoa maelezo na kutangaza kumuondoa kocha Michel aliyekuwa ameletwa mwaka jana kuziba pengo la kocha Marcelo Bielsa aliyejiuzulu.


Katika kipindi cha miezi 8 ya ukufunzi wake, Michel ameweza kushinda mechi 8 pekee na timu ya Olympique Marseille jambo ambalo ni kinyume na matarajio.


Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Olympique Marseille itaendelea kuwa chini ya kocha msaidiziFranck Passi hadi mwishoni mwa msimu huu.

No comments: