Sunday 17 April 2016

Sergio Aguero aididimiza Cheslea kwa kuifunga goli 3


Manchester City yatembeza kichapo kwa Cheslea nyumbani

 Manchester City yatembeza kichapo kwa Cheslea nyumbani

Timu ya Manchester City ilisafiri mjini London kupambana na Chelsea kwenye mechi ya ligi kuu ya soka ya EPL nchini Uingereza.

 

Licha ya kucheza nyumbani, Chelsea ilishindwa kuleta faraja mbele ya mashabiki wake na badala yake, wakapokea kichapo kikali cha 3-0 kutoka kwa Manchester City.

 

Mshambuliaji matata wa Manchester City Sergio Aguero ndiye aliyefunga magoli yote matatu mojawapo likiwa ni kupitia mkwaju wa penalti.

 

Kwa matokeo hayo, Manchester City wameweza kukusanya jumla ya pointi 60 baada ya kucheza mechi 33.

No comments: