Monday 11 April 2016

TOTTENHAM YATEMBEZA KICHAPO KIKALI KWA MANCHESTER UNITED


Timu ya Manchester United ilisafiri ugenini kwenda kutoana jasho na Tottenham Hotspur kwenye mechi yao ya ligi kuu ya EPL nchini Uingereza.

Timu hizo mbili pinzani zilikabiliana vilivyo katika kipindi cha kwanza na kuelekea mapumzikoni kwa sare ya 0-0.

Katika kipindi cha pili, wenyeji Tottenham Hotspur walizidisha mashambulizi na kufanikiwa kuvunja ngome ya ulinzi ya Manchester United.


Hatimaye Tottenham Hotspur ikafanikiwa kuitandika Manchester United bao 3-0 na kuondoka na pointi 3.

No comments: