Monday 11 April 2016

LIVERPOOL YAINYESHEA STOKE CITY MVUA YA MAGOLI EPL



Timu ya Liverpool iliikaribisha Stoke City nyumbani Anfield kwenye mechi ya ligi kuu ya soka ya EPL nchini Uingereza.

Liverpool ambayo bado inajivuta kuwania nafasi ya kuingia 4 bora kwenye ligi ya EPL, ilikuwa sababu ya kutabasamu kwa kufanikiwa kuondoka na pointi 3.

Wageni Stoke City walipokea kichapo cha Liverpool kwa kucharazwa bao 4-1 kwenye mechi hiyo.

Kwingineko, viongozi wa ligi Leicester City nao waliendeleza msururu wao wa ushindi baada ya kuwashinda Sunderland bao 2-0.


Ushindi huo umewawezesha Leicester City kuendelea kujikita kileleni huku matumaini yao ya kushinda taji la EPL yakizidi kuongezeka.

No comments: