Tuesday 24 May 2016

MESUT ÖZIL AZURU MAKKAH KWA AJILI YA KUTEKELEZA IBADA YA UMRAH


Mesut Özil azuru Makkah kwa ajili ya kutekeleza ibada ya umrah
Kiungo wa kati wa Ujerumani anayechezea kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Mesut Özil, amezuru mji mtukufu wa Makkah nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya umrah.

 
Mesut Özil ambaye siku chache zilizopita alichaguliwa mchezaji bora wa Arsenal msimu huu, alisambaza picha alizopiga Makkah kwenye akaunti yake ya mtandao wa jamii wa Twitter.


Maelfu ya mashabiki wa Mesut Özil wanaomfuatilia kwenye mitandao ya jamii walivutiwa mno na picha hizo alizosambaza mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid.


Kutokana na ustadi wake aliouonyesha msimu huu na kilabu ya Arsenal, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kwa ajili ya kucheza kwenye mashindano ya EURO 2016 nchini Ufaransa.

No comments: