Wednesday 18 May 2016

WARRIORS WAGONGA MWAMBA MECHI YA KWANZA YA PLAY-OFF NBA


Oklahoma City Thunder ilikutana na Golden State Warriors kwenye mechi ya kwanza ya Play-Off  ya fainali ya Western Conference NBA.

Mabingwa watetezi wa taji la NBA Warriors, waligonga mwamba kwa kushindwa na Thunder vikapu 108-102.

Nyota wa Thunder Russell Westbrook na Kevin Durant waliibeba timu yao kwa uchezaji mzuri na kufunga vikapu 27 na 26 mtawalia.

Na katika upande wa Warriors, MVP wa NBA Stephen Curry alifunga vikapu 26 ingawaje haikutosheleza kuipindua Thunder.


Kufuatia ushindi huo, Thunder imeweza kuongoza msururu wa Play-Off 1-0 dhidi ya Warriors.

No comments: