Meneja wa timu ya taifa
ya Uingereza Roy Hodgson amemtaja chipukizi wa Manchester United Marcus
Rashford kwenye kikosi chake cha wachezaji watakaocheza Euro 2016.
Rashford, 18, alianza
kuchezea timu kuu ya Uinted kipindi cha pili cha msimu lakini aliwika mara
moja.
Alifunga mabao manne
mechi zake mbili za kwanza na aliwafungia mabao saba katika mechi 16 tangu
aanze kuwachezea 25 Februari.
Hodgson ametaja kikosi
cha wachezaji 26, ambacho kitapunguzwa baadaye hadi wachezaji 23.
Winga wa Newcastle United
Andros Townsend na kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere pia wamo kwenye
kikosi hicho kitakachopigania ubingwa Ufaransa, kwenye michuano hiyo
itakayoanza tarehe 10 Juni.
Siku ya mwisho kwa
mataifa 24 yanayoshiriki kutangaza timu zao za wachezaji 23 ni tarehe 31 Mei.
Kikosi
Walinda mlango: Joe
Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).
Mabeki: Gary Cahill
(Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle
Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham
Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).
Viungo wa kati: Dele
Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Manchester
City), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan
Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool),
Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle United), Jack
Wilshere (Arsenal).
Washambuliaji: Wayne
Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy
(Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester
United).
No comments:
Post a Comment