Thursday 25 February 2016

BASEBALL WAFANYA BONANZA LA AINA YAKE



Wanafunzi kutoka Skuli mbali mbali visiwani Zanzibar wametakiwa kushiriki katika michezo tofauti ,ili kuweza kujenga mwili pamoja na kuweka akili sawa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa wa Elimu Mafunzo ya Amali Mkoa wa Mjini Magharibi Khatib Tabia ambae alikuwa mgeni rasmi katika bonanza maalum la mchezo wa Baseball Uliyofanyika uwanja wa Magereza Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja.

Tabia alisema michezo ni njia moja wapo wa ajira sanjari na kuleta mahusiano mazuri na jamii.

“Michezo ni ajira, michezo ni afya, ukishiriki michezo afya yako lazima iwe nzuri, musisubiri mpaka Daktari akuambie ufanye mazoezi, leo nimefurahi sana kuja kwenye bonanza hili maana nilikuwa nauwona kwenye TV tu mchezo huu wa Baseball leo nimefurahi nimeuwona Live kwa kweli ni mchezo mzuri”.

Nae mwenyekiti wa chama cha baseball Zanzibar Abdul halim SHIMAOKA mwenye asili ya Japan alitowa taarifa fupi kuhusu historia ya mchezo huo ulipoanzishwa Zanzibar.

“ Tulianza shule ya Mwanakwerekwe na Dole Disemba, 2014 na Mwaka huo huo tukashiriki mashindano ya Tanzania ambayo yalifanyika kule Dar es salam, ukweli kwa muda mfupi tumepanda daraja kubwa kuliko hata Tanzania Bara na mwaka 2016 tutachukua Ubingwa”. Alisema Shimaoka.

Jumla ya timu 5 zilishiriki katika bonanza hilo Maalum la baseball timu ambazo ni Mwanakwerekwe C, Youth Star, Kidoti, Langoni na Ndijani ikiwa ndizo timu pekee visiwan Zanzibar wanaocheza mchezo huo.

No comments: