Monday 28 March 2016

MAJIMAJI WAJIPIMA NGUVU YA UWEZO WAKE KWA MARANYENGINE TENA.





Ligi daraja la kwanza taifa Pemba hatua ya sita bora inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo miwili katika Uwanja wa Gombani.

Wakati wa saa nane mchana timu ya News Star ambayo ilikubali kupokea kibano cha magoli  4 – 1 kutoka timu ya Danger Boys ya Kangani katika mchezo uliyochezwa Ijumaa itakutana tena na timu ya Majimaji ya Tumbe ambayo nayo ilipokea kibano cha magoli 4 – 0 siku ya jumamosi na Chuo/Basra.

Chuo/Basra  yenyewe leo hii inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Mkungu Malofa ambayo ilitoka sare ya bila bila katika mchezo uliyopita na timu ya Wawi Star ambapo hapo kesho Wawi Star wataikaribisha timu ya New Star wakati wa saa kumi za jioni katika uwanja wa Gombani.

Hadi sasa ligi hiyo ambayo timu tatu za juu zitapanda ligi kuu Zanzibar inaongezwa na Wawi Star yenye alama 7 wakishinda michezo miwili na kutoka sare mmoja ikifuatiwa na Chuo /Basra yenye alama 6 kwa kushinda michezo miwili na kufungwa mmoja.

Nafasi ya tatu  mpaka sasa inshikiliwa na Danger Boys  yenye alama 4 baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare mmoja na kufungwa mmoja.
Nafasi ya nne ni News Star yenye alama 3 sawa na Majimaji yenye alama 3 pia huku timu ya Mkungu Malofa ikishika mkia katika ligi hiyo kwa kua na alama 2 baada ya kucheza michezo mitatu.


Timu zote zimebakiwa na michezo miwili kukamilisha hatua hiyo. 

No comments: