Tuesday 23 February 2016

JEROME CHAMPAGNE MKOMBOZI MPYA WA AFRIKA KOMBE LA DUNIA?


FIFA itakuwa na rais mpya ifikapo tarehe 26 February 2016. Baada ya miaka 18 ya utawala wa Sepp Blatter ambao umegubikwa na utata mwingi hasa shutuma za rushwa na ubadhilifu pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, Utawala wa Blatter utafikia mwisho katika kikao cha FIFA kitakachofanyika Zurich Uswisi.
Wagombea watano wanawania kiti hicho cha kuwa mtu mkubwa katika utawala wa Soka duniani na kwa yeyote yule atakayeshinda kiti hicho basi atakuwa Rias wa tisa wa kuchaguliwa katika historia ya miaka 112 ya FIFA.
Rais wa FIFA atachaguliwa kwa kura zitakazopigwa na wanachama 209 wa FIFA isipokuwa Kuwait na Indonesia ambao wamefungiwa  kwa maana hiyo kutakuwa na kura207 tu za kugombaniwa
Afrika kuna kura 54, Ulaya kura 53, Asia kura 46 Kaskazini na Amerika ya kati pamoja na visiwa vya Carribean kura 35, Ocenia kura 11 na Amerika ya kusini kura 10. Mgombea yeyote anahitaji theluthi mbili ya kura zote  kupita katika raundi ya kwanza.
Baada ya hapo katika hatua zinazofuata mgombea mwenye kura chache anatoka katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA.
Kuelekea uchaguzi wa Rais mpya wa FIFA huu ndio uchambuzi wa kina kuhusu Mgombea Jerome Champagne
JEROME CHAMPAGNE:
Anasimamia wapi?
Kama ilivyo kwa mgombea mwenza Prince Alli, Jerome Champagne aligombea katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei lakini hakupata kura za kumuunga mkono kutoka kwa Nchi wanachama lakini hivi sasa amefanikiwa kupata kura za kuungwa mkono na amepiga kampeni za kutosha kuhakikisha anachukua kiti cha Urais wa FIFA na kurudisha heshima ya soka pale inapotakiwa kuwa.
Champagne amefanya kazi FIFA kwa miaka 11 mpaka pale alipofukuzwa na Blatter, ambapo kwa kipindi chote hicho Blatter amekuwa katika shutuma nzito pamoja na chuki dhidi ya rais wa soka bara la Asia Mohammed Bin Hammam.
 Ana Nafasi gani ya Kushinda?
 Kimsingi hana nafasi kubwa ya kushinda lakini anaweza kusema mawazo yake yana mchango mkubwa sana katika mjadala huu toka mwanzo wa kampeni, alitabiri huu utakuwa uchaguzi wa uhuru na wazi “Huu mgogoro ni wa hatari sana. Vyama vyote vya soka vinataka mtu mwenye uzoefu wa kutosha . Sijali kama sina nafasi”.
“(Barack) Obama hakuwa na nafasi, Papa Francis hakuwa na nafasi, Francois Hollande hakuwa na nafasi. haya ndiyo maisha”
Japokuwa anaweza asipate nafasi ya kuwa Rais wa FIFA Champaige anaweza kurudi FIFA katika nafasi ya utawala ana uchu na ujuzi wa kuwa Katibu mkuu wa FIFA.
Atakuwa Rais wa aina gani?
Champaigne amesema atafanya mambo makuu matatu kama atachaguliwa: kumbusu mke wake, Kufungua chupa ya Champaigne na mwisho  kwenda kusherehekea siku inayofuata ataingia kazini na kuanza kuitengeneza FIFA mpya.
Alisema atakuwa Rais wa kuongoza kwa vitendo kwa maana atafanya kazi kwa vitendo huku akiwashutumu wapinzani wake kwa kutaka kuwa marais wanaotaka heshima.
Chmpaigne anayatambua vizuri mazingira ya FIFA baada ya kuwa amefanikiwa kufanya kazi kama mshauri wa Rais wa FIFA Sepp Blatter na Katibu mkuu msaidizi lakini pia amefanya kazi kama Mkurugenzi wa Uhusiano wa kimataifa.
Kabla ya kuingia FIFA alikuwa mwandishi wa habari, mwanadiplomasia wa Ufaransa na mkuu wa itifaki wakati wa kombe la Dunia mwaka 1998.
Kipi anachojivunia?
Itakuwa taarifa mbaya kwa bara la Ulaya kama Champaigne atachukua madaraka ya Urais wa FIFA kwa sababu mipango yake ni kutoa nafasi chahce za nchi za Ulaya kushiriki katika fainali  za kombe la Dunia, kwa sasa Ulaya ina nchi wanachama 53 ambao wana nafasi 13 huku Afrika ikiwa na Nchi wanachama 54 lakini ikiwa na nafasi tano tu.
Champaigne amesema kunahitajika usawa katika suala hili na haamini kama usawa huo unatokana na kuongeza timu shirikikutoka 32 mpaka 40.
kitu kingine anataka kuifanya FIFA iwe ya uwazi na kuharakisha mipoango ya maendeleo kuongeza kasi na hadhi katika mashindano ya soka kwa wanawake, na kuruhusu matumizi ya teknolojia ya video kuwasaidia marefarii katika maamuzi.
Champaigne anataka kuzidisha mara mbili bajeti amabayo huwa inatolewa kwa nchi 100 wanachama ambao ni masikini  kutoka euro 170,000 kwa mwaka mpka 340,000 kwa mwaka.
na atahamisha kombe la dunia litakalofanyika Qatar mwaka 2022 kutoka kipindi cha joto mpaka majira ya mwezi wa tano na wa sita.
 Anafikiria nini kuhusu Sepp Blatter?
Hana tatizo na Blatter licha ya kuwa alimfukuza kazi FIFA, Champaigne anaamini Blatter ni kiongozi mzuri aliyefanya maamuzi mabovu katika utawala wake: “Kama tunavyotambua hakuhusishwa na ufisadi. Naamini historia itamuelezea tofauti kuliko taarifa hizi zilizopo sasa. Hakuna mtu anayeweza kusema kuwa Blatter amefanya mapinduzi katika soka”.
Champaigne na Blatter bado wana uhusiano mzuri licha ya Blatter kumtimua Champaigne kazi FIFA.
shaffih dauda

No comments: