Wednesday 9 March 2016

Washindani wa kwanza wa robo fainali ya ligi kuu ya UEFA kubainika


Timu mbili za kwanza zitakazofuzu robo fainali ya ligi kuu ya vilabu bingwa barani Ulaya ya UEFA watabainika leo hii.

Katika mechi za marudiano, Real Madrid itaikabili Roma katika uwanja wa Santiago Bernabeu nchini Uhispania.

Roma itakuwa na kibarua kigumu cha kuipindua Real Madrid ambayo iliweza kushinda mechi ya kwanza 2-0.

Kwingineko Wolfsburg nayo itapambana na Gent nchini Ujerumani. Katika mechi ya kwanza, Wolfsburg iliondoka na ushindi wa 3-2.

Mechi zote zitang'oa nanga mwendo wa saa 21.45 usiku kwa nyakati za Uturuki.

No comments: