Wednesday 2 March 2016

YANGA YATUA VISIWANI PEMBA KWA MATAYARISHO YA MCHEZO KATI YAO NA AZAM FC




Timu ya Yanga ya Dar-es Salaam ambayo imewasili visiwani Pemba hapo jana kwa kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya timu ya Azam FC siku ya Jumamosi leo tayari imeanza kufanya mazoezi kisiwani humo.

Yanga ambayo wakati wa asubuhi ilafanya mazoezi yake katika fukwe za bahari zilizopo katika hoteli waliyofikia ya Pemba Misali Sunset iliyopo Wesha nje ya kidogo ya mji wa Chake Chake lakini pia walilazimika kufanya mazoezi wakati wa saa nane za mchana kijua kikiwaka uwanja wa Gombani kutokana na jioni kuwepo kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza taifa Pemba kati ya Masota Rangers na Cossovo ya Wambaa.

Hata hivyo mazoezi hayo ambayo yakuhudhuriwa na mashabiki wengi kama ilivyozoeleka kutokana na mashabiki hao kujongea katika uwanja wa Gombani wakati wa saa kumi za jioni wakidhani kuwa Yanga watafanya mazoezi wakati huo.

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba kesho timu hiyo itafanya mazoezi yake wakati wa asubuhi kwenye uwanja wa Gombani na saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo ambapo michezo ya ligi daraja la kwanza kisiwani humo sasa itachezwa wakati wa saa nane za mchana.

Uongozi wa timu ya Yanga umesema kwa sasa hawatatoa taarifa zozote juu ya mazoezi yao visiwani hapa hadi siku ya Ijumaa watakapozungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha kambi yao visiwani humo.

No comments: