Thursday 28 April 2016

BAYERN MUNICH YAAMBULIA PATUPU NUSU FAINALI YA UEFA, WACHARAZWA 1-0 NA ATLETICO

Atletico Madrid v Bayern Munich

Bayern Munich yaambulia patupu ugenini kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la UEFA

Nusu fainali ya pili ya ligi kuu ya kilabu bingwa barani Ulaya ya UEFA iliwakutanisha Atletico Madrid na Bayern Munich katika uga wa Vicente Calderon.

Bayern Munich waliokuwa wakicheza ugenini walikuwa na wakati mgumu kupenyeza kwenye ngome ya ulinzi ya Atletico Madrid na kushindwa kupata goli.
 

Wenyeji Atletico Madrid walileta faraja kwa mashabiki wao kwa kupata goli la pekee lililofungwa na Saul Niguez katika dakika ya 11 na kuletea ushindi wa 1-0.


Mechi ya marudiano itachezwa siku ya Jumanne tarehe 3 Mei katika uga wa Allianz Arena nchini Ujerumani.

No comments: