Wednesday 13 April 2016

CHIPUKIZI NA MWENGE WAONJA JOTO YA JIWE



KAMPENI "FICHUA VIPAJI"

Timu za Chipukizi na Mwenge ambazo zilikuwa hazijawahi kufungwa tokea kuanza kwa ligi kuu ya Zanzibar Kanda ya Pemba msimu huu jana zilionja machungu baada ya kupekea vipigo.

Chipukizi ambazo imeshinda katika michezo yake mitatu ya kwanza ilijikuta ikilala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Young Islanders katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani.

Young Islanders walitangulia kupata bao katika lakika ya 54 lililofungwa na mchezaji wake Abdulrahman Hassan, hata hivyo mshambuliaji machachari wa Chipukizi Abdulkarim Ali aliisawazishia timu hiyo katika dakika ya 70.

Bao la ushindi la Young Islanders liliwekwa wavuni na Salim Ali Salim kwenye dakika ya 77.

Na hadi dakika 90 za mwamuzi Suleiman Kisauti zinamalizika Young Islanders 2 na Chipukizi 1.

Katika uwanja wa FFU Finya timu ya Mwenge ya Wete nayo ikijikuta chali mbele ya timu iliyonekana kibonde kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye michezo yake mitatu ya kwanza kwa kupata sare 1 tu Okapi ya Msuka kwa kuchapwa bao 1-0.

Na katika mchezo baina ya FSC na Aljazira uliochezwa kwenye uwanja wa Kangani Skuli timu ya FSC imeibuka na ushindi wa magoli 3-1.


Leo ndiyo leo pale viwanja vyote vitatu vitakapowaka moto FFU Finya kukiwa na Hardrock na Kizimbani, Kangani Skuli itakuwa ni kati ya Dogomoro na African Kivumbi na Gombani Shaba iliyojeruhiwa kwenye mchezo uliopita watakuwa na wakongwe Jamhuri.

No comments: