Wednesday 13 April 2016

WHITE BIRD YACHAPWA 2-1 NA CHWAKA


Timu ya White bird imekubali kichapo cha mabao 2-1 walipocheza na Chwaka katika muendelezo wa ligi daraja la kwanza taifa kanda ya Unguja hatua ya sita bora, mchezo ambao uliovurumishwa ndani ya dimba la Amani mjini Unguja.

Katika mchezo huo ulikuwa wa kasi kwa timu zote kwani kila timu ilitaka kupata ushindi katika mchezo huo ili kujiwekea nafasi nzuri ya kuweza kupanda ligi kuu, ndipo Chwaka walipoanza kuandika bao la kwanza kupitia mchezaji Ridhwan Moh’d katika dakika ya 67.

Timu hizo ziliendeleza mashambulizi na ilipofika dakika ya 81 Bernad Lukas akaipatia Chwaka bao la pili, lakini dakika mbili tu baada ya bao hilo White bird nao walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Issa Shomari katika dakika ya 83 ya mchezo huo,na mchezo huo ulimalizika kwa Chwaka kuondoka na alama tatu katika mchezo huo.

Akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA kocha wa timu ya White bird Moh’d Abdul-kadir amesema kuwa,

“Mechi ilikuwa ni nzuri bahati tu imekuwa mbaya kiupande wetu, ndo mchezo kwa sababu sisi tumetumia nafasi tumeshindwa kuzitumia, wenzetu wametengeneza nafasi wameshinda kuzitumia, makosa tumeyaona na tutayafanyia kazi”. Alisema kocha Abdul-kadir.

Vilevile tulizungumza  na kocha wa timu ya Chwaka Issa Mjanakheir amesema kuwa licha ya kushinda lakini mchezo ulikuwa ni mgumu.

“Mchezo mgumu lakini nimeshinda namshukuru Mungu. Tatizo tuliloliona tutarudi mazoezini tutalirekebisha kwa sababu mechi bado mbili kwa hiyo tatizo hulo tumeliona na tuatalifanyia kazi, Mungu akipenda ni maandalizi tu kama tulivojiandaa mechi zote ni maandalizi tu ili tushinde mechi nyengine”. Alisema kocaha Mjanakheir.

Matokeo hayo yameifanya timu ya Chwaka kuwa kileleni wakiwa na alama tano (5), na White bird wao wapo nafasi ya nne (4) na alama tatu (3)

No comments: