Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU, imeendeleza dimbwi lake la ushindi baada ya kuwanyuka Kimbunga mabao 3-0, katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa jana ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.
Katika mchezo huo
uliochezwa majira yan saa kumi za jioni, JKU walianza kucheza kwa kasi na
kwenda kulishambulia lango la Kimbunga ndipo Emmanuel Martin alipofunga bao la
kwanza katika dakika ya pili (2).
JKU iliendeleza
mashambulizi na kuutawala mchezo huo takriban dakika zote za kipindi cha kwanza,
pia walikosa nafasi nyingi za kushinda lakini katika dakika ya 44 Mbarouk
Chande alifunga bao la pili, na kuweza kujiandikia bao la kumi (10) katika ligi
hiyo huku akimfukuzia mchezaji wa Kimbunga Shomari Waziri mwenye mabao 12,
ambae mchezo wa jana hakuonesha makali yake kama ilivyozoeleka.
Mnamo dakika za
nyongeza za kipindi cha kwanza Emmanuel Martin alirudi tena wavuni kwa
kuiandikia JKU bao la tatu (3).
Katika kipindi cha pili
Kimbunga waliimarisha safu yao ya ulizi kwani hawakuruhusu bao jengine katika
lango lao, na mtanange huo ulimalizika kwa JKU kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Kocha wa timu ya JKU
Omar Khamis kuwa wamtengeza nafasi nyingi katika mchezo huo lakini wamezitumia
kidogo.
“Tumetengeza nafasi
nyingi lakini tumezitumia kidogo lakini nyingi zaidi tumezikosa, kwa kweli haya
yote ni kutokuwa makini, kwa sababu nafasi kama zile tungezipata tungeweza
kufunga magoli kirahisi kabisa”. Alisema Omar.
Kwa upande wa Kaimu
kocha wa timu ya Kimbunga Ali Khamis Tall, amesesma kuwa “kutokana na kufungwa
magoli matatu kwa kweli hali ya timu yangu mumeiona hata reserve hakuna
wachezaji wengi ni wagonjwa, sasa wachezaji wenyewe nimelazimisha tu kucheza”.
Kwa matokeo hayo JKU
bado ni vinara wa ligi hiyo, wakiwa na alama 44, na Kimbunga wao wana alama 23
wakishika nafasi ya tisa (9).
No comments:
Post a Comment