Timu ya polisi bado ipo
katika wakati mgumu katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya jana
kutoka sare ya bila ya kufungana walipocheza na majeshi wa Kipanga katika
mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni.
Licha ya timu hizo
kucheza mchezo mzuri lakini walizipoteza nafasi nyingi ambazo wamezipata kwani
wachezaji hao hawakuwa makini kabisa katika umaliziaji wao, na kupelekea
kumalizika kwa mtanange huo bila ya bao lolote kwa pande zote.
Ali Suleiman Mtuli,
kocha wa timu ya Polisi amesema kuwa, “Tatizo kama mlivoliona bado sijawa
makini katika kuzitumia nafasi, tunapata nafasi nyingi, timu inatengeneza
nafasi nyingi sana lakini bado tunapoteza nafasi, icho ndo kilio chetu Polisi
kwa sasa”.
Aidha Mwenyekiti wa
timu ya Kipanga Meja Shamhuna amesema, “Mechi ya leo vijana wamecheza vizuri
wamejitahidi na tumetengeza nafasi nyingi tu lakini kwa bahati mbaya ma forward
hawakuzitumia vizuri, na hiyo inatokana na part of the game unaweza unaweza
ukapata nafasi nyingi na msizitumie au mkapata nafasi moja mkaitumia hiyo hiyo,
ni hali ya mchezo”.
Kwa matokeo hayo
Kipanga wamefikisha alama 24 wakiwa nafasi ya nane 8, na Polisi wapo nafasi ya
pili kutoka chini ambayo ni nafasi ya kumi na tatu 13 na alama kumi 10.
No comments:
Post a Comment