Vijana wa kocha
Benjamin Ayimba waliandikisha historia hiyo kwa kuichapa Fiji alama 30 kwa 7
katika fainali iliyokuwa ikitazamiwa na wengi.
Alama za Kenya
zilifungwa na Samuel Oliech kisha nahodha na mfungaji nambari mbili duniani
Collins Injera akafanya mambo kuwa 10-0.
Oscar Ayodi Nelson Oyoo
na kisha Frank Wanyama akaihakikishia Shujaa kombe lake kuu la kwanza katika
ligi ya raga ya kimataifa ya IRB.
Kenya imeshiriki katika
mashindano 114 ikitafuta ushindi huu.
Sadfa ni kuwa japo timu
hiyo ndiyo timu ya pekee katika msururu huo wa IRB inayosheheni wachezaji wasio
wa kulipwa ilijifurukuta na kuwalaza mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo
ya IRB Fiji .
Kenya ambayo
inaorodheshwa katika nafasi ya 8 duniani sasa imejizolea alama 22 na kuipiku
Uingereza kutoka nafasi ya 7 na alama 85.
'Shujaa' Kenya
inavyojulikana ilianza kuonesha dalili za ufanisi mapema katika msururu huo wa
Singapore ilipoilaza Argentina 15-12 ,katika hatua ya nusu fainali.
Hiyo ndiyo iliyokuwa
mara kwanza kwa Kenya kufuzu nusu fainali tangu mwaka wa 2013.
No comments:
Post a Comment