Monday 18 April 2016

Leicester yabanwa mbavu EPL.


Vinara wa ligi kuu ya England walishindwa kuutumia vyema uwanja wao nyumbani wa King Power kwa kukubali sare ya mabao 2-2 na West Ham .

 Leicester Citys Jamie Vardy, No 9, walks off the pitch after being sent off during the English Premier League soccer match between Leicester City and West Ham United at the King Power Stadium in Leicester, England, Sunday, April 17, 2016. (AP Photo/Rui Vieira)

Jamie Vardy, aliipa Timu yake uongozi kwa bao la kwanza katika dakika ya 18, mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll,akasawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati kabla ya Aaron Cresswell kuongeza bao la pili kwa upande wa Wagonga nyundo.

 

Katika dakika ya lala salama Jose Leonardo Ulloa akaisawazishia Leicester kwa goli la mkwaju wa penati.

Matokeo hayo bado  Leicester wanaendelea kushika uongozi wa ligi hiyo wakiwa  na alama 73, wakati West Ham wao wapo nafasi ya sita 6 na alama 53.

No comments: