Saturday 16 April 2016

KUMEKUCHA LIGI KUU TANZANIA BARA.



Ligi Kuu Tanzania bara inaendelea tena leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.Huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

 

Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar mchezo utaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.

 

Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

No comments: