Monday 23 May 2016

BAYER LEVERKUSEN YAMSAJILI CHIPUKIZI WA HOFFENHEIM

Kevin Volland atia saini mkataba wa miaka mitano na kilabu ya Bayer Leverkusen

Kilabu ya Bayer Leverkusen kutoka Ujerumani imetangaza kumsajili mshambuliaji chipukizi Kevin Volland aliyekuwa akichezea Hoffenheim.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya Bayer Leverkusen, iliarifiwa kwamba Kevin Volland alitia saini mkataba wa miaka mitano.

Vyanzo vya habari nchini Ujerumani vinaarifu kwamba Kevin Volland alitia saini mkataba huo kwa dau la fedha Euro milioni 18.

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani  mara 6, alifunga jumla ya magoli 8 kwenye mechi 33 alizochezea Hoffenheim msimu uliopita.

No comments: