Sunday 22 May 2016

SERVET TAZEGÜL ASHINDA NISHANI YA DHAHABU KATIKA MASHINDANO YA TAEKWONDO

Servet Tazegül ashinda nishani ya dhahabu katika mashindano ya taekwondo

Mwanaspoti Servet Tazegül apeperusha bendera ya Uturuki kwenye mashindano ya taekwondo barani Ulaya

Servet Tazegül ambaye ni mshiriki wa taekwondo, aliibuka mshindi barani Ulaya kwenye mashindano ya 22 ya tekwondo yaliyoandaliwa mjini Montro nchini Uswisi.

Servet Tazegül aliyekuwa akiwakilisha Uturuki kwenye mashindano hayo ya Ulaya, alishinda nishani ya dhahabu katika kitengo cha washiriki wa kiume wa uzani wa kilo 68.

Katika mashindano hayo, Servet Tazegül aliwashinda Boriz Ruizi wa Andora 3-2 , Ben Haines wa Uingereza 6-2 na Viacheslav Minin wa Urusi 9-7 kwenye raundi ya pili, tatu na robo fainali mtawalia.

Katika hatua ya nusu fainali, Servet Tazegül alimshinda Konstantin Minin wa Urusi 15-5 na kutinga fainali kwa kishindo ambapo alipambana na mjerumani Hamza Adnan-Karim mwenye asili ya Turkmenistan.

Servet Tazegül aliibuka bingwa baada ya kushinda fainali hiyo 6-5 na kuweza kunyakuwa nishani ya dhahabu kwa mara ya 5 ikiwa ni pamoja na mwaka 2008,2010,2012 na 2014.

Kwa upande wa wanawake, Zeliha Ağrıs wa Uturuki pia aliweza kushinda nishani ya shaba kwa washiriki wa uzani wa kilo 53.

Zeliha Ağrıs alimshinda Tatiana Kudashova wa Urusi 10-6 kwenye fainali ya kuwania nafasi ya tatu.

No comments: