Sunday 22 May 2016

MANCHESTER UNITED WALINYAKUA KOMBE LA FA




Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezwa uwanja wa Wembley.

Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.

Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata katika dakika ya 81 na Jesse Lingard dakika ya 110.

Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon dakika ya 78.

Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.

Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.

"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema Van Gaal.

No comments: