Shirikisho la soka duniani FIFA limeishtumu Afrika Kusini kwa
kulipa hongo ya dola milioni 10 ili kupewa fursa ya kuandaa kombe la dunia la
mwaka 2010,kulingana na ripoti ya gazeti la Telegraph nchini Uingereza.
Fifa ilitoa ''taarifa ya mwathiriwa'' na ''ombi la kurudisha
fedha'' hizo kwa afisi ya wakili wa Marekani,gazeti hilo limeongezea.
Maafisa wa Afrika Kusini wamesisitiza kuwa hawakulipa hongo.
Fifa inajaribu kukomboa makumi ya mamilioni ya fedha
zilizochukuliwa kinyume cha sheria na wanachama wa shirikisho hilo pamoja na
mashirika mengine ya soka.
Maafisa wa zamani wa shirikisho hilo Chuck Blazer na Jack
Warner pamoja na Jeffery Webb ni miongoni mwa wale waliofunguliwa mashtaka na
Fifa ambayo imewasilisha stakhabadhi kwa mamlaka ya Marekani.
Fifa imekuwa katika mgogoro tangu madai ya ufisadi kugunduliwa
mnamo mwezi Mei 2015.
Kwa jumla watu 41 pamoja na kampuni kadhaa zimeshtakiwa na
mamlaka ya Marekani.
Uchunguzi wa Marekani ulifichua ufisadi mkubwa katika
shirikisho hilo na Fifa inakadiria kwamba mamilioni ya madola yaliibwa kupitia
hongo,kiinua mgongo na mipango ya ufisadi iliofanywa na washtakiwa.
BBC.
No comments:
Post a Comment