Saturday 12 March 2016

BINGWA MTETEZI MAFUNZO KUCHUANA NA KIPANGA. JE! NANI ZAIDI KATI YA TIMU HIZI AMBAZO ZINACHUANA KATIKA MSIMAMO ZIKIWA NA ALAMA SAWA?


Mshikemshike wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja ukiendelea kushika nafasi yake,leo majira ya saa kumi za jioni Wazee wa jelajela timu ya Mafunzo ambao ni bingwa mtetezi watachuana vikali na Majeshi wa Kipanga.
 Mchezo huo utasukumwa ndani ya dimba la Amani hapa visiwani Zanzibar, ambapo mashabiki pamoja na kikosi cha  Mafunzo wakitarajia timu yao kupata ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kulitetea taji lao.
Kwa upande wa wanajeshi wa kipanga nao hawatokuwa nyuma katika mchezo huo, kwani na wao pia wapo katika harakati za kuwania ubingwa msimu huu, hivyo wataingia uwanjani kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wake ili waondoke na lama tatu katika mchezo huo.
Mafunzo na Kipanga wote wana alama sawa 22, wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa lakini Mafunzo wao wapo nafasi ya saba (7), na Kipanga nafasi nane (8).
Je, nani zaidi kati ya timu hizi,Kipanga atazidi juu ama Mafunzo au watabakia kuwa sawa kwa alama?
Usikose kuuangalia mtanange huu wa kukata na shoka wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja katika uwanja wa Amani hapa mjini Unguja majira ya saa kumi za jioni.

No comments: