Saturday 12 March 2016

WAAMUZI WA SOKA NCHINI NDIO KIZINGITI KWA SOKA LA TZ



Wadau na wachezaji wa soka nchini wamelalamikia juu ya ukuaji wa soka nchini wakisema kiwango cha ukuaji wake hakiridhishi kabisa na kwamba juhudi kubwa inahitajika kufanyika.

Wamesema, kadiri ya siku zinavyosonga mbele badala ya kwenda mbele ndio kiwango kinavyorudi chini  ingawa katika hali ya juujuu kinaonekana kukua lakini sio uhalisia wenyewe.

Wakiongea na SALMA SPORT’SMEDIA kwa nyakati tofauti wadau wa soka nchini wameonesha kutoridhidhwa na mazingira ya uchezeshwaji wa ligi wakisema umejaa mapungufu ndio sababu kuu inayo pelekea kutokukua kwa soka la Tz  kasi zaidi.

Mmoja miongoni mwa waliokua wachezaji walioichezea timu ya Mvomerou wiliya,  timu ya Morogoro katika ligi ya kill taifa Cup na  Police Morogoro ligi daraja la kwanza msimu wa 2014 -2015 Salumu Juma amesema kutokana na uwendeshaji mbovu wa ligi za tz inapelekea timu nyingi kutopiga hatua mbele “soka la Tz ukuaji wake hauridhishi kwa kiasi kikubwa na hili linatokana na uwendeshwaji wake mbovu wa ligi zetu”alisema Juma.

Amesema waamuzi wanafanya maamuzi yao binafsi na bado wapo wanaendelea na kazi zao hali ambayo inarudisha nyuma na inakatisha juhudi za wachezaji.

Akitoa mchango wake juu ya nini kifanyike ili kukuza soka letu ameiomba TFF  iboreshe ligi za daraja la kwanza kwani ndio zinazoonesha vipaji vya wachezaji kwa haraka sana pamoja na kuwaandaa vizuri waamuzi wa michezo hiyo.

Pia ameishauri TFF  ianzeshe vituo vingi vya soka nchini kwaajili ya watoto kwani wengi wanajitihada kucheza soka lakini wanashindwa na wapi pakukimbilia, amesema kufanya hivyo kutasaidia kuibua vipaji katika nchi yetu.

Nae  mildifild na mshambuliaji wa timu ya Ruvu shooting  ligi daraja la kwanza Mkoa wa pwani  Ayoub Kitala akizungumzia juu ya changamoto zinazolikabili soka la Tanzania amesema kitu kikubwa kinachochangia soka kushuka ni waamuzi wasiozingatima maadili ya kazi zao “soka la bongo marefa ndo wanaosababisha soka lichelewe kukua haraka kwa sababu wengine wanachezesha huku wakiwa na yao moyoni”alisema Kitala

Amesema waamuzi wengi katika uchezeshaji wao wanazibeba timu  ambazo hazina uwezo hali ambayo imeelezwa kua kufanya hivyo huko mbele ndio kunakua na timu kubwa mbovu.


No comments: