Bingwa mtetezi,timu ya Mafunzo imejipa matumaini ya kuingia hatua ya nne bora kwa upande wa Unguja, na kulitetea taji lao la ligi kuu ya Zanzibar.
Timu hiyo imeweza
kufufua matumaini yao baada ya kuwafunga Maustadh wa Chuoni bao 1-0 katika
mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya dimba la
Amani hapa mjini Unguja.
Mafunzo imejipatia bao
hilo lililofungwa na Moh’d Abdul-Rahiim Mbambi katika dakika ya 60 muda mchache
tu alipotokea bench kwa kuchukua nafasi ya Ali Juma.
Kocha wa timu ya
Mafunzo Moh’d Kachumbari amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri na kila mtu kaonesha
uwezo wake.
“Mchezo ulikuwa mzuri
tu kila mtu kaonesha uwezo wake lakini sie tulikuwa tunatumia sana upande wa
ushambuliaji kwa sababu timu yetu sasa hivi tupo katika mambo ya umaliaziaji,
tumepata goli moja lakini tumeondoka na ushindi”.Amesesma Kachumbari.
Kachumbar aliongezeza kwa kusema, “tunafanya mazoezi
kuingia katika timu za nne bora tumekusudia safari hii kuuchukua tena ubingwa
kwa njia ya aina yoyote ile”.
Kwa upande wa kocha wa
Chuoni Abdallah Ali, amesesma
“Mchezo tumepoteza
kwanza marifa wanazibeba sana za askari,kwa sababu tumefunga goli clear refaree
anasema hamna goli. Kupoteza mechi ni kama mechi ya kawaida,tumecheza ingawa
kipindi cha kwanza walituzidi lakini kipindi cha pili tulicheza sawasawa na
bahati ikawa yao wamepata ushindi”.
Timu ya Mafunzo sasa
wamefikisha alama 29 wakiwa nafasi ya nne 4, na Chuoni wapo nafasi ya kumi 10 na
alama 22.
No comments:
Post a Comment