Friday 11 March 2016

SHANGANI YAIZABUA LEEDS UNITED 3-1


Katika mchezo wa ligi daraja la pili wilaya Mjini uliosukumwa jana ndani ya dimba la Amani mjini Zanzibar Leeds United wamekubali kichapo cha mabao 3-1walipofungwa na Shangani.

Mabao ya Shangani yamefungwa na  Ali Khamis katika dakika ya 20 na dakika 47 na bao jengine limewekwa kimyani na Salum Omar mnamo dakika ya 24.

Lakini kwa upande wa Leeds United bao la kufutia machozi limefungwa na Omar Rashid katika dakika 15.

Nahodha wa timu ya Leeds United Muhamad Issa amesema kuwa tatizo kubwa la kufungwa ni kutokana na kuchoka sana kutokana na kutokuwepo kwa mazoezi ya pamoja,pia amesema jua kali ndio tatizo jengine lilopelekea kupoteza mchezo huo.

“tumefungwa kwa sababu ya kuchoka na wao sio wazuri, timu yetu haina mazoezi ya pamoja kwa hiyo kila mmoja anacheza kwa uwezo wake binafsi,ushirikiano ni mdogo tunacheza mechi jua kali na pia mazoezi ya pamoja hatuna”. Alisema Muhamad Issa.

Aidha  kocha wa timu ya Shangani Suleiman Hamid amesema kuwa, mchezo ulikuwa ni mzuri kwani wanacheza kutokana na mazingira ya jua kali katika sehemu wanazofanyia mazoezi,

“mchezo ulikuwa hali nzuri tu kwa sababu sisi tulikuwa tunacheza kwa mujibu ya mazingira ya hali ya hewa iliyokuwepo na uwezo wetu, kwa sababu tulikuwa tunajitahid kumiliki mpira ili kuweza kutokana na hali halisi kutokana na wakati mbaya wa jua kali, kwa hiyo tumecheza vizuri na mechi ilikuwa nzuri” Alisema kocha Suleiman Ole.

Aliendelea kwa kusema,“Kwa kweli tulikuwa tunafanya mazoezi kwa sababu sisi tuna malengo ya kuingia katika hatua ya nane bora kwa hiyo ili kuweza kuingia ni kuhakikisha kwamba mechi hii tunashinda ili kuishinda ni kufanya mazoezi, kutokana na hali ya mazingira sisi tunafanya mazoezi saa nane lakini pia tunacheza kwa hali halisi ya kiwanja nacho kinaunguza, kwa hiyo tumecheza na wachezaji wamepokea maagizo ambayo wamepewa”.Alisema kocha Suleiman .


Katika mtanage huo kikosi cha Shangani wamevaa jezi rangi ya blue, huku Leeds United wakiwa wamevaa jezi nyeupe.

No comments: