Friday 11 March 2016

MSHAMBULIAJI WA NEW FLAMINGO ACADEMY : NITAPAMBANA MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU


KAMPENI  "FICHUA VIPAJI"

Mshambuliaji wa timu ya New Flamingo Academy ya Dar es salaam Fadhili Abdallah amesema ingawa changamoto ni nyingi sana katika kabumbu lakini atapambana mpaka tone la mwisho la damu kuhakikisha anazishinda changamoto zilizombele yake mpaka kufikia alichokikusudia na si chengine zaidi ya kusifika kwa soka ndani na nje ya taifa.

Ameyasema hayo jana alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA katika kampeni maalum ya “FICHUA VIPAJI”

Abdallah amesema mara nyingi amekua akifanya mazoezi ya kujituma katika timu yake ili ailetee mafanikio na hata mwenyewe kujiweka katika mazingira mazuri ya uchezaji bora.

SALMA SPORTS MEDIA  imeshuhudia hali za wachezaji wa timu hiyo zikiwa si za kuridhisha kutokana na uhaba kumbwa wa vifaa.

Mipira ya kuchezea ni michache na iliyo katika hali mbaya, aidha vifaa kama vile viatu n ahata nguo za mazoezi nazo pia ni majanga.


Katika mazungumza na wachezaji wa timu hiyo ya kiwango cha Junior wamewaomba wahisani kujitokeza kuwadhamini ili matumaini yao yafikie pazuri kwani wanauwezo mzuri wa kucheza soka.

No comments: