Friday 11 March 2016

TOTTENHAM WAKIRI KUWA WALIHARIBU GAME WENYEWE.


Kutokana na matokeo mabovu iliyoyapata timu ya Tottenham kwenye mechi yao ya ugenini dhidi ya Borussia Dortmund kocha wake amekiri kuwa waliharibu gemu hiyo.

Mauricio Pochettino kocha wa timu hiyo amesema “timu yangu haikucheza vizuri kwenye mechi yetu ya ugenini dhidi ya Borussia Dortmund kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora.”

Alieleza “ni vigumu kueleze lakini hii ni siku mbaya kwetu na nimesikitishwa sana na kiwango chetu. Hatukucheza vizuri ndiyo maana tukapoteza game, tunahitaji kupambana kwenye mchezo wetu wa marudiano wiki ijayo. Kipigo cha bao 3-0 siyo mazuri kwetu lakini tunahitaji kuendelea kupambana na kujaribu Alhamisi ijayo”.

“Hii ilikuwa ni mechi yetu ya kwanza kupoteza kwa bao 3-0 msimu huu. Tunahitaji kutulia na kuhakikisha haijirudii tena”.

Spurs ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 3-0 ugenini huku wachezaji wenye uzoefu kama Eric Dier, Harry Kane, Mousa Dembele na Erik Lamela wote wakianzia benchi kwenye mechi hiyo.

Magoli ya Dortmund yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alifunga goli la kwanza kwa kichwa wakati Reus yeye akalipiga msumari jahazi la Spurs kwa kufunga bao mbili zilizokamilisha ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya wageni Spurs.


Watu wengi wanajiuliza kwamba, kuwapumzisha wachezaji hao ni kwa ajili ya mechi ya Premier League kati ya Spurs dhidi ya vibonde Aston Villa?

No comments: