Monday 28 March 2016

Rwanda kushuka dimbani Kigali AFCON

Timu ya taifa ya Rwanda itashuka dimbani kesho ikilenga kufufua kampeni yake ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.
Rwanda watakuwa wenyeji wa Mauritius kwenye mechi yao ya marudiano Kundi H.
Amavubi walilazwa 1-0 na wanavisiwa hao Jumamosi iliyopita na watahitaji sana kushinda kufufua matumaini yao.
Mkufunzi wao mkuu Jon McKinstry amesema ana matumaini kwamba wanaweza kufanya mambo dhidi ya Les Dodos.


“Kila mtu amesikitishwa na matokeo (ya mechi ya Jumamosi). Lazima tuwe wakweli na kukubali kwamba hatukucheza vyema,” amesema kocha huyo.
Ghana wanaongoza Kundi H baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Msumbiji ugenini Maputo Jumapili, kila timu ikiwa imecheza mechi nne.
Mauritius wamo nambari mbili na alama sita, pointi tatu juu ya Rw
bbc

No comments: