Wednesday 30 March 2016

SERENA WILLIAMS ACHUJWA MIAMI OPEN


Mkali wa tenisi kutoka Marekani Serena Williams amezidi kuyumba katika ulingo wa tenisi kwa matokeo yasiyoridhisha.

Serena Williams ambaye ameanza vibaya mwaka huu, amekosa taji la Miami Open baada ya kushindwa kufuzu robo fainali.

Bingwa huyo mtetezi wa taji hilo alibanduliwa na Svetlana Kuznetsova katika raundi ya 3 baada ya kushinda seti 2-1 za msururu wa 7-6, 1-6 na 2-6.


Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Serena Williams ameshindwa kubeba mataji matatu ikiwa ni pamoja na Australian Open na BNP Paribas Open alizocheza fainali.

No comments: