Monday 11 April 2016

BARCELONA YAPOTEZA POINTI UGENINI DHIDI YA REAL SOCIEDAD



Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya La Liga nchini UhispaniaBarcelona walisafiri ugenini kupambana na Real Sociedad kwenye mechi yao ya wiki ya 32.

Wageni Barcelona walikuwa na wakati mgumu dhidi ya wenyeji Real Sociedad na kushindwa kutikisa wavu ndani ya dakika 90.

Real Sociedad walileta faraja kwa mashabiki wake baada ya kupata goli la pekee lililofungwa na Mikel Oiarzabal katika dakika ya 5.


Goli hilo la pekee lililetea Real Sociedad pointi 3 huku Barcelona ikirudi nyumbani mikono mitupu.

No comments: