WAZAZI wametakiwa kuondoa dhana potofu ya kwamba mwanafunzi
akishiriki michezo Skuli hushusha kiwango cha ufahamu wa masomo yake darasani .
Mratibu wa michezo Wilaya ya Micheweni mwalimu Ali Nassor
amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya elimu na michezo kwani michezo hukuza kipaji cha mwanafunzi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , mwalimu Ali
amewataka wazazi kuondoa vizuizi kwa watoto wao bali wawape fursa na muda wa
kutosha kushiriki michezo .
Aidha amefahamisha kwamba watoto wengi wamepata ajira kupitia
michezo , na kuwaeleza kuwa kuna tofauti kubwa ya ufahamu wa mwanafunzi
ayeshiriki michezo na asiye shiriki michezo .
Mwalimu Ali pia amewasisitiza wazazi kujenga utamaduni wa
kufuatilia maendeleo ya watoto wao , na kuacha kukaaa majumbani na kutupa
lawama wa walimu na kamati za skuli pekee.
Naye mwalimu Zawadi Amour Nassor amesema kuwa walimu
wameandaa ratiba ambayo itamfanya mwanafunzi kushiriki michezo bila ya kuathiri
ratiba ya vipindi vyake vya masomo darasani .
No comments:
Post a Comment