Timu ya Kikosi Maalum
cha Kuzuia Magendo KMKM imekubali kubamizwa kichapo cha mabao 2-0 walipocheza
na Kikosi cha Valantia Zanzibar KVZ katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda
ya Unguja.
Mabao ya KVZ yamewekwa kimyani na Salum Songoro katika dakika
ya 35, na bao la pili limefungwa na Suleiman Hassan mnamo dakika ya 89 ya
mchezo huo.
Kocha wa KMKM Ali Bushir Mahmoud amesema kuwa wachezaji wake
hawakucheza kama alivyowafundisha.
“Mchezo wa leo tumepoteza kwa kweli wachezaji wangu
wameniangusha, sijawahi kusema kitu icho lakini nathubutu kusema kwamba vijana
wangu wameniangusha kwa sababu kipindi ambacho tulikuwepo katika matayarisho ya
mchezo huu tulifanya mabo mengi sana ambayo leo sikuona hata moja katika yale
ambayo tumefanya hawakufanya kabisa wamecheza mpira sio kabisa, sasa nathubutu
kusema kwamba wachezaji wangu wameniangusha kabisa”. Alisema kocha Bushiri.
“Nimepata ushindi ambao sikuutegemea kwa sababu mechi ya
kwanza KMKM waliweza kunifunga kwa mabao 2-1 kwa hiyo leo nimekuja kwamba vipi
nitaweza kupigana na timu ya KMKM na nashukuru Mungu kwamba nimeweza kushinda
mabao 2-0”. Alisema kocha King.
Matokeo hayo yameifanya KVZ kuwa na alama 33 na kubaki nafasi
yao ya pili, huku KMKM wakibaki nafasi yao ya nne na alama 27.
No comments:
Post a Comment