Sunday 3 April 2016

MAFUNZO YAINYUKA KIMBUNGA 3-0



Katika mcchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliochezwa leo ndani ya dimba la Amani mjini Unguja bingwa mtetezi wa ligi hiyo timu ya Mafunzo imeondoka na alama tatu muhimu baada ya kuwanyuka kimbunga mabao 3-0.

Mchezo huo uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni Mafunzo walianza kujipatia bao la kwanza kupitia mchezaqji  Mohd Abrahman katika dakika ya 23.

 Na timu hizo ziliukwenda mapumziko Mafunzo wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila.

Timu ziliporudi kumaliza ngwe ya lala salama  kila timu ilitaka kuondoka na alama tatu siku ya leo na ndipo Wazee wa jela jela timu ya Mafunzo wakapata bao la pili liliwekwa kimyani na Shaban Ali mnamo dakika ya 68, na Ali Othman Mmanga ndiye aliyewamaliza kabisa timu ya Kimbunga baada ya kuipatia Mafunzo bao la tatu katika dakika ya 76 ya mchezo huo.

Na mtanange huo ulimalizika kwa Mafunzo kuondoka na ushindi mnene wa mabao 3-0.

Kwa matokeo hayo timu ya Mafunzo imefikisha alama 26 wakiwa nafasi ya saba (7), huku Kimbunga wao wakiwa nafasi ya nane (8) na alama 23.

No comments: