Sunday 3 April 2016

KAFI ZA WAZEE WA DAGO ZAPIGA UWANJA WA GOMBANI, MIZINGA YA HARDROCK YAGOMA KUFANYA KAZI.



Na Is-haq Muhammed Pemba

Wazee wa Dago timu ya Shaba imeanza kufanya yake baada ya leo kuipangua mizinga ya Hardrock katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliopigwa kwenye Uwanja wa Gombani Pemba.

Hardrock ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli kupitia kwa mchezaji wake Elius Laisome katika dakika ya 10 bao ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

Kuanza kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ili kuimarisha vikosi vyao.

Hata hivyo mabadiliko hayo yalionekana kuwanufaisha Shaba kwa kufanya mambo katika dakika 45 za kipindi cha lala salama.

Suleiman Juma ndiye aliyelikomboa bao kwa kuisawazishia timu yake ya Shaba kwenye dakika ya 64.

Na mnamo dakika ya 72 mchezaji Kombo Bakar ambapo katika dakika ya 89 alipachika bao la tatu na kuamsha shangwe uwanjani hapo na ngoma maarufu ya Charanga ikirindima katika uwanja huo.

Na hadi dakika 90 za mwamuzi Moh`d Seif akisaidiwa na Mwadini Ali na Saidi Ali zinamalizika Shaba 3 na Hardrock 1.


Ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba itaendelea kesho Jumatatu katika viwanja viwili, ambapo kwenye uwanja wa Gombani FFS watakipiga na Sharp Victor na Jamhuri iliyojeruhiwa na Chipukizi kwa bao 1-0 katika mchezo wake wa kwanza watakuwa na Aljazira wenyewe wakipokea kichapo kitakatifu cha magoli 4-1 kutoka kwa kizimbani.

No comments: