Monday 4 April 2016

San Antonio Spurs yavunja rekodi ya ushindi.

Timu ya San Antonio Spurs yajiwekea rekodi mpya ya ushindi NBA

Timu ya San Antonio Spurs inayocheza kwenye ligi kuu ya mpira wa kikapu ya NBA nchiniMarekani, imejiwekea rekodi mpya ya ushindi.
Spurs ilifanikiwa kuweka rekodi mpya kwa kushinda jumla ya mechi 64 ndani ya msimu mmoja wa ligi ya NBA.
Spurs ilifikia rekodi hiyo mpya baada ya kuishinda Toronto Raptors kwa vikapu 102-95 hapo jana.
Kwa sasa zimebakia mechi 6 ili msimu wa NBA wa mwaka huu ukamilike, hivyo basi, Spurs huenda ikaendelea kujiwekea rekodi hiyo zaidi hadi mwishoni mwa msimu.

No comments: