Monday 4 April 2016

JKU KUENDELEA KUCHEZA VIPORO VYAKE NA BOYS LEO JIONI.


Wakati ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja ikiendelea kutimua vumbi lake hapa visiwani Zanzibar leo timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) wataendelea kucheza mechi zake za viporo ambapo leo watachuana vikali na Jang’ombe boys.

Katika mtanange huo utakaosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni, kila timu ikiwa na hamu ya kutaka kupata ushindi  ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuingia hatua ya nne bora kwa upande wa Unguja.

JKU wataingia uwanjani wakiwa bado wanaongoza ligi hiyo kwa kanda ya Unguja wakiwa wana alama 35, huku Jang’ombe boys wao wakiwa nafasi ya 11 na alama 18.

No comments: