Wednesday 11 May 2016

MAFUNZO WAZIDI KUWADIDIMIZA MTENDE LIGI KUU ZANZIBAR.

Bingwa mtetezi wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya Mafunzo wamezidi kuwaweka mkiani Mtende Rangers baada ya kuwacharaza mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya dimba la Amani mjini Unguja.

 

Katika mchezo huo Sadik Habib alianza kuiandikia Mafunzo bao la kwanza mnamo dakika ya 36, bao ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

Mafunzo walijipatia bao la pili katika dakika ya 76 kupitia mchezai  aliyetokea bench Rashid Abdalla ambae amechukua nafasi ya Kheir Salum, na mchezo kumalizika kwa Mafunzo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtende.

Kocha wa timu ya Mtende Abrahman Mussa, amezungumza na SALMA SPORT’S MEDIA na amesema mchezo ulikuwa mzuri lakini matokeo yao bado sio mazuri.

 “Mchezo mzuri lakini matokeo yetu bado sio mazuri,sasa hivi tunamatatizo kwa upande wa wachezaji, wachezaji wetu sasa hivi kidogo wameondoka, kwa hiyo  hapa tunakuja tuna wachezaji 10, 12, moja kati yam abo ambayo yanasababisha tusifanye vizuri, kama wachezaji wetu watarudi basi tutafanya vizuri”. Alisema kocha Abrahman.

Aidha kocha wa timu ya Mafunzo Moh’d Shaaban Kachumbar, amesesma wamekuja washinde ili wakamate nafasi za juu na waingie katika hatua ya nne bora.

“Tumekuja tushinde mechi ya leo ili tukamate nafasi ya pili tuingie hatua ya nne bora, tukibahatika kuingia hatua ya nne bora kwa timu yangu mm ninavyoijua Mafunzona mwalimu wetu mkuu alokuwepo basi tunahakikisha kupigana kuchukua ubingwa wa Zanzibar”. Alisema Kachumbar.

Matokeo hayo yameipandisha Mafunzo hadi nafasi ya tatu (3) wakiwa na alama 35, na Mtende wanashika mkia wakiwa na alama kumi (10).

No comments: