Wednesday 30 March 2016

HATIMAE SHARRIF JUMA SAID ATANGAZA NIA YA KUWANIA NAFASI YA MAKAMO WA RAIS WA ZFA TAIFA.


Mjumbe wa ZFA Taifa kupitia Wilaya ya Chake Chake Sharrif Juma Said ametangaza nia ya kujitosa kuwania nafasi ya Makamo wa Rais wa ZFA Taifa kwa upande wa Pemba katika uchaguzi wa ZFA uliopangwa kufanyika tarehe 9, April.

Sharrif  amesema kuwa ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kwa kile anachodai anatosha kushika nafasi hiyo kutokana na kuwa na uwezo wa kuongoza nafasi hiyo.

Alisema amekuwa mchezaji na kiongozi wa siku nyingi wa mpira kwa nyakati tofauti na hiyo inampa sifa ya kuchaguliwa kuwa miongoni mwa viongozi wa awamu ijao ya chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA).


Sharrif anakuwa mwanamichezo wa kwanza kutia nia ya kuwania nafasi ya makamo wa Rais wa ZFA Taifa Pemba katika uchaguzi wa mwaka huu ambapo pia nafasi hiyo inategemewa kutetewa na makamo wa Rais wa sasa Ali Mohammed Ali.

Msikilize Said anavyozungumza katika mahojiano na mwanamichezo wetu kutoka Pemba Is-haq Muhammed


No comments: