Monday 25 April 2016

MAHREZ MCHEZAJI BORA WA MWAKA UINGEREZA PFA 2015-16.



 Mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya chama cha wachezaji soka ya kulipwa Uingereza (PFA).

Mahrez amefunga mabao 17 na kusaidia katika ufungaji wa mengine 11 katika mechi 34 za ligi alizochezea Leicester na kuwasaidia sana kukaribia kushinda taji la ligi.


Mahrez ni raia wa Algeria.

Wachezaji soka ya kulipwa Uingereza ndio hupiga kura kuamua mshindi.

 
Kiungo wa kati Tottenham Dele Alli, mwenye umri wa miaka 20, ndiye aliyeshinda tuzo ya PFA ya mchezaji chipukizi wa mwaka naye mshambuliaji Izzy Christiansen akashinda tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka.


Mshambuliaji wa Sunderland Beth Mead, mwenye umri wa miaka 20, ndiye aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa kike.

No comments: