Sunday 24 April 2016

MANCHESTER UNITED YATINGA FAINALI KOMBE LA FA.

Manchester United yaitandika Everton 2-1 na kuingia hatua ya fainali kwenye kombe la FA


Nusu fainali ya kwanza ya kombe la FA nchini Uingereza ilichezwa kati ya Manchester United na Everton katika uga wa Wembley.
 Manchester United yatinga fainali kombe la FA

Timu hizo mbili zilitoana jasho ili kuwania nafasi kwenye fainali ya kombe la FA.


Manchester United ilitangulia kupata goli la kwanza lililofungwa na Fellaini katika dakika ya 34 kabla ya beki wao Chris Smalling kujifunga katika dakika ya 76 na kusawazishia Everton.


Baada ya vuta nikuvute ya dakika za mwisho, Manchester United ilifanikiwa kupachika goli la pili kupitia Anthony Martial aliyefunga katika dakika ya 90 na kuihakikishia ushindi.

 
Sasa Manchester United itasubiria mpinzani wake wa fainali ya kombe la FA atakayebainika hapo kesho kati ya Crystal Palace na Watford.

No comments: