Saturday 23 April 2016

MILIONI 10 KWA TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA RAGA YA KENYA

Shilingi milioni 10 kwa timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya



Mabingwa wa raga nchini Kenya watunukiwa shilingi Milioni 10 na rais Uhuru Kenyatta

Siku ya Alhamis rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikuwa mwenyeji wa washindi wa timu ya kitaifa ya mchezo wa raga katika ikulu ya rais mjini Nairobi.

 

Mabingwa hao wa Kenya Sevens Rugby​ walirudi nchini Kenya siku ya Jumanne baada ya kuibuka washindi katika michuano ya raga roundi ya nane ya mchezo wa raga​ HSBC​ World.

 

Nahodha wa timu hiyo ya kitaifa Andrew Amonde​ alimkabidhi rais Uhuru kombe la ushindi .

 

Akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo,rais Uhuru Kenyatta alitangaza tuzo la shilingi milioni 10 kwa timu hiyo kutoka kwa serikali ya Kenya kama shukrani kwa mashujaa hao kwa kuendelea kupeperusha bendera ya Kenya Kimataifa.

 

Aidha mbali na tuzo hilo rais Kenyatta aliongezea kuhakikishia kuwa udhamini wa timu hiyo utaendelea kuimarishwa.

 

Aliambia timu hiyo waendelee kufanya mazoezi bila ya kuchoka na serikali itaendelea kutoa misaada ili kutayarisha kuwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki.

 

 

 

No comments: