Sunday 15 May 2016

JUVENTUS YAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA SERIE A.


Mabingwa wa ligi ya Serie A Juventus wamaliza msimu kwa kishindo.
Juventus yakabidhiwa rasmi kombe la Serie A
Kilabu ya Juventus iliyotawazwa mabingwa wa ligi ya Serie A nchini Italia wiki iliyopita, walimalizia mechi yao ya mwisho msimu huu nyumbani dhidi ya Sampdoria.

Mabingwa hao watetezi waliweza kutembeza kichapo kikali kwa wageni Sampdoria kwa kuwanyeshea mvua ya magoli 5 bila jibu.

Baada ya mechi hiyo ya msimu wa mwaka 2015-2016, Juventus walikabidhiwa rasmi kombe la Serie A.

Juventus pia imeweza kujiwekea rekodi mpya kwa kuwa timu ya kwanza kufanikiwa kuchukuwa ubingwa wa Serie A mara tano mfululizo kwa awamu mbili tofauti.

Timu nyingine zilizowahi kunyakuwa taji la Serie A mara tano mfululizo ni Torino katika miaka ya 1943, 1946, 1947, 1948 na 1949, na Inter katika miaka ya 2006, 2007, 2008, 2009 na 2010.

No comments: